Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha
Abstract & Details
Research Area
Educational
Keywords
-
Abstract
Ubadilikaji wa lugha na udumishaji wa lugha ni mada ambazo kwa muda mrefu sasa zimewavutia wataalamu mbalimbali wa Isimujamii. Makala haya yalishughulikia udumishaji wa Kirombo yakiwa na lengo la kuchunguza kama lugha hii inadumishwa au la. Lengo la makala haya lilikuwa kubaini nani anatumia Kirombo na nani anatumia Kiswahili kwenye maeneo teule ya matumizi katika kudumisha lugha na kuhitimisha kama Kirombo kinadumishwa au la. Ili kufikia lengo hili watafiti walitumia mbinu za hojaji, mahojiano na ushuhudiaji katika kukusanya data. Aidha, utafiti huu uliongozwa na mkabala wa kinadharia wa uchanganuzi wa kimaeneo kama ulivyotumiwa na Fishman (1972). Nadharia hii inaelezea mazoea ya watu ya kupenda kuchagua lugha fulani itumike katika eneo fulani na lugha nyingine itumike katika eneo jingine, mazoea ambayo hufungamana na utamaduni wa jamii inayohusika na hujengwa na kudumishwa na wazungumzaji wenye utamaduni mmoja na lugha moja. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba udumishaji wa lugha ya Kirombo upo kwa kiasi kidogo ambapo unafanywa zaidi na wazee huku watu wa rika la kati na vijana wakitumia zaidi Kiswahili katika maeneo yote ya matumizi yaliyoteuliwa, hali inayohatarisha kutoweka kwa lugha ya Kirombo kwa vizazi vijavyo. Matokeo haya yamedhihirisha kuwa upo ubadilikaji wa lugha ya Kirombo unaoendelea kuelekea zaidi katika lugha ya Kiswahili. Makala haya yamependekeza hatua mbalimbali za kuchukua ili kunusuru lugha hii isipotee kabisa. Baadhi ya mapendekezo hayo ni pamoja na asasi za serikali, za dini, asasi mbalimbali za lugha, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla kusisitiza umuhimu wa kuzungumza lugha ya asili, hasa kwa vijana ambao hawaoni fahari kuzungumza lugha yao ya Kirombo.
License
This work is licensed under a Creative
Commons
Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
Author Information
| # | Name | Institute / Affiliation |
|---|---|---|
| 1 | Eva E. Mongula | Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan, Morogoro, Tanzania |
| 2 | Peter T. Mramba | Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan, Morogoro, Tanzania |
How to Cite
Use the following formats to cite this article in your research.
APA Style
Mongula, Eva E. & Mramba, Peter T. (2025). Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha. International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education, 11(4), 599-613.
MLA Style
Mongula, Eva E., and Peter T. Mramba. "Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha." International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education, vol. 11, no. 4, 2025, pp. 599-613.
IEEE Style
Eva E. Mongula and Peter T. Mramba, "Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha," International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education, vol. 11, no. 4, pp. 599-613, 2025.
Vancouver Style
Mongula Eva E., Mramba Peter T.. Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha. International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education. 2025;11(4):599-613.
Harvard Style
Mongula, Eva E. & Mramba, Peter T. (2025) 'Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha', International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education, 11(4), pp. 599-613.
Chicago Style
Mongula, Eva E. and Peter T. Mramba. "Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha." International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education 11, no. 4 (2025): 599-613.
Turabian Style
Mongula, Eva E. and Peter T. Mramba. "Kuchunguza Nani Anazungumza Kirombo au Kiswahili kwenye Maeneo Teule ya Matumizi katika Kudumisha Lugha." International Journal of Advance Research and Innovative Ideas In Education 11, no. 4 (2025): 599-613.
Related Research
A Qualitative Inquiry on the Department of Education’s Induction Program for Beginning Teachers (IPBT) from the Lens of Mentors And Mentees
PDF Unavailable
Leading with Integrity: A Qualitative Inquiry on How School Heads Model Professional Conduct
PDF Unavailable
MANAGEMENT STRATEGIES TOWARD TEACHERS’ INTERPERSONAL CONFLICT
PDF Unavailable
Policy in Practice: Role strain Experiences of head Teacher Amid Administrative shifts
PDF Unavailable
CHANGE MANAGEMENT STRATEGIES AND ORGANIZATIONAL CULTURE AS PREDICTORS OF SCHOOL PERFORMANCE
PDF Unavailable
PREDICTING ENGLISH GRAMMAR PROFICIENCY THROUGH LANGUAGE EXPOSURE AND TEACHER EFFECTIVENESS
PDF Unavailable